Sunday, November 19, 2017

MANCHESTER UNITED 4-1 NEWCASTLE UNITED, POGBA ARUDI NA BAO OLD TRAFFORD. LUKAKU, MARTIAL NA SMALLING WAKITUPIA NYAVUNI PIA LEO.

Romelu Lukaku akirukiwa na  Antonio Valencia baada ya kuipachikia bao la nne Man United usiku wa leo hii kwenye Ligi Kuu England. Man United wamefunga bao 4-1.
Lukaku akimfunga kipa wa Newcastle
Lukaku  akiwanyanyua mashabiki Old Trafford
Zlatan Ibrahimovic leo nae karudi na kuwasha cheche


Paul Pogba akiziona nyavu za Newcastle United leo hii Old Trafford

Bao

Shangwe kwa Pogba kurudi kwake na bao
Chris Smalling nae alijitwisha na kufunga bao

Mara Paap

Bao
Anthony Martial aliisawazishia bao Man United
Mlinda mlango Rob Elliot akiushangaa mpira mara baada ya kuzama nyavuni

PICHA ZA HARUSI YA SERENA WILLIAMS ZAANZA KUONEKA KWA MARA YA KWANZA


Gauni kali alilovaa bibi harusi Serena Williams limeweza kuonekana kwa mara ya kwanza katika picha kadhaa zilizotolewa baada sherehe ya harusi usiku wa Alhamisi na mumewe muasisi wa mtandao wa Reddit Alexis Ohanian.
Picha za tukio hilo ambalo chombo pekee cha habari kilichopewa ruhusa ya kupiga tukio hilo ni jarida la Vague, zinamuonyesha Williams akiwa amependeza vilivyo katika siku yake hiyo muhimu iliyohudhuriwa pia na mtoto wao mchanga.


Maharusi Serena Williams na mumewe Alexis Ohanian wakiwa katika pamoja na ndugu wa karibu wa familia zoa

Wageni waalikwa nyota mbalimbali wakipiga makofi kuwashangilia maharusi Serena na Ohanian.

KOCHA MKUU WA KILI STARS YA CHALENJI ALIYETANGAZWA LEO

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Ammy Ninje kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ ambayo inajiandaa na mashindano ya Chalenji ambayo yanatarajiwa kuanza Desemba 3-17 Nairobi.
Akizungumza leo wakati akimtambulisha, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema kocha huyo kesho anatarajiwa kutangaza kikosi kitakachoshiriki michuano ya kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.
“Ninje siyo mgeni kwenu mmemuona kwenye benchi la Taifa Stars takribani michezo miwili, hivyo ndio atakayekiongoza kikosi cha Kilimanjaro Stars kwenye mashindano ya Chalenji yatakayofanyika Nairobi,” alisema Lucas.
Akizungumza baada ya kutambulishwa, Ninje alisema kazi ya kocha siyo kuongea bali ni kuonesha kwa vitendo kile kilichomo ndani yake, nakuomba ushirikiano kwa wadau ili timu atakayotangaza leo ifanye vizuri na hatimaye itwae kombe la Chalenji.
“Nashukuru kwa TFF kuniamini na kunikabidhi timu ya Kilimanjaro Stars ambayo imepangwa kundi A pamoja na timu za Libya, Rwanda na wenyeji Kenya,” alisema Ninje ambaye ni kocha mwenye leseni A ya UEFA.
Kabla ya kuwa kocha Ninje aliwahi kucheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini 1996 timu za Hellenic FC na baadae Wynberg St Jones kabla ya kujiunga na Sparta Rotterdam (Mutual) FC ya China pia alicheza katika nchi za Denmark, USA, Scotland na England.
Kwa sasa Ninje mwenye taaluma ya Uhasibu anafundisha timu ya Vijana ya klabu za Hull City na Notts County na baadhi ya wachezaji maarufu waliwahi kupitia katika mikono yake ni Josh Tymon, Josh Clackstone, Harvey Rodgers, Dan James, Max Clarke, Colby Bishop, Lartey Sarpong, Luther Wilder, Jack McMillian, Montel Gibson, Alex Penny, Jordan Richards, Harry Caldwell na Rory Watson.

TFF YAKANUSHA HABARI ZA KUONGEZWA POSHO, KUWABURUZA MAHAKANI WALIOSAMBAZA HABARI HIYO

Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao (wa pili kushoto) akizungumza na wandishi wa habari leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Wanachama na Sheria, Edward Mwakingwe, Mkurugenzi wa Mashindano Efrem August na Mkurugenzi wa Masoko Aaron Nyanda

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema litawachukulia hatua za kisheria watu ambao wataeneza na kusambaza habari ambazo hazina ukweli kuhusu shirikisho hilo.
Hayo yamesemwa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao wakati akitoa ufafanuzi wa ujumbe/habari iliosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuongeza posho kwa wajumbe wa kamati ya utendaji pamoja na kuanzisha malipo ya mishahara kwa Rais na Makamu wake.
Kidao alisema viwango vya posho za vikao vya Kamati ya Utendaji havijawahi kujadiliwa wala kubadilishwa (kuongezwa) tangu uongozi mpya uingie madarakani bali kamati ilipitisha posho y ash. Milioni 1.5 kwa wajumbe kwa miezi mitatu ili iwasaidie kutekeleza majukumu yao.
“Wajumbe wa kamati ya utendaji wanawezeshwa kutekeleza majukumu yao kwenye kanda zao kwa kulipwa sh. Milioni 1.5 ambayo ni sawa na laki tano kila mwezi na hii posho anapewa baada ya kuwasilisha taarifa ya kazi ambazo amezifanyaka katika kipindi cha miezi mitatu kwenye kanda yake,” alisema Kidao.
Kidao alisema kuhusu mshahara wa Rais wa TFF na Makamu wake hilo halikufikiwa mwafaka kwani halikufuata taratibu japo wajumbe wa kamati ya utendaji walishauri ofisi ya Rais ihudumiwe na TFF kama ilivyo kwa ofisi za marais wa FIFA na CAF.
“Rais wa TFF Wallace Karia alikataa kwa kusema, anaamini sio wakati mwafaka wa yeye kuchukua posho hadi taasisi itakapokaa vizuri na taratibu zote kufuatwa na pia yeye ni mtumishi wa serikali hawezi kupokea mshahara miwili kwa wakati mmoja,” alisema Kidao.
Kidao ambaye katika mkutano huo alikuwa ameambatana na wakurugenzi wapya akiwemo Mkurugenzi wa Wanachama na Sheria, Edward Mwakingwe alimwagiza kuanza kufanya taratibu za kuwafikisha mahakama watu wote waliosambaza taarifa hiyo kwani ina lengo la kuichafua taasisi hiyo.
“Nakuagiza mwanasheria wa TFF, kufungua mashtaka kwa wale waliosambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii wenye lengo la kuichafua taasisi hiyo kwani sheria ya mitandao inakataza kusambaza habari ambazo zinalengo la kuchafua na kuharibu twasira ya taasisi,” alisema Kidao.
Pia Kidao alisema ofisi yake ipo wazi muda wote endapo kuna habari wanataka kupata ufafanuzi wasisite kumpigia na endapo wataona simu haipokelewi watu ujumbe mfupi maana inawezekana akawa yupo kwenye kikao.
Katika kikao hicho aliwatambulisha wakurugenzi wapya ambao ajira zao zilipitishwa na kamati ya utendaji ambao ni Mkurugenzi wa Wanachama na Sheria, Edward Mwakingwe, Mkurugenzi wa Masoko Aaron Nyanda, Mkurugenzi wa Mashindano Efrem August na Mkaguzi wa ndani John Benjamin

Wednesday, November 8, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI WA WILAYA YA MISENYI NA KUTEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI CHA KAGERA SUGAR, MISENYI MKOANI KAGERA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Wilaya ya Misenyi(hawaonekani pichani) wakati akielekea katika kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Wilayani hapo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiandika wakati wananchi wa Misenyi walipokuwa wakiwasilisha Kero zao mara baada ya kusimama wakati akiwa njiani kuelekea katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo wialayani humo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa kwa shangwe na Mamia ya wananchi wa Misenyi mara baada ya kuwasili Wialayani hapo akitokea Bukoba mjini.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasikiliza wananchi wa Misenyi wakati wakitoa kero zao mbalimbali mara baada ya kuwasili.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akizungumza katika eneo hilo la Misenyi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wa pili kutoka kushoto , Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba wa kwanza (kulia) wakisikiliza mtaalamu wa Kilimo (haonekani pichani) aliyekuwa akielezea mambo mbalimbali katika mashamba ya miwa katika Kiwanda hicho cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Misenyi mkoani Kagera.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Shamba la miwa la Kiwanda hicho cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Misenyi mkoani Kagera


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Mitambo ya kuchujia na kuvutia maji kwa ajili ya Mashamba ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar, mitambo hiyo ipo pembezoni mwa Mto Kagera katika Wilaya ya Misenyi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mbegu na mbolea inayotumika katika mashamba hayo ya miwa ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar kilichopo Misenyi mkoani Kagera.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja katika Mashamba hayo ya miwa na viongozi wa Kiwanda hicho cha Sukari cha Kagera Sugar, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wa kwanza kulia akifatiwa na Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Viwanda Charles Mwijage wa kwanza kulia.

. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi (Vibarua) wanaofanyakazi katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera Sugar wakati akielekea kiwandani hapo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua baadhi ya mashamba hayo ya miwa ya Kiwanda cha Kagera Sugar kilichopo Wilayani Misenyi mkoani Kagera. PICHA NA IKULU

BEN POL AWAAMSHA WABUNGE VITINI KWENYE TAMASHA LA TIGO FIESTA DODOMA


Wabunge wa bunge la Tanzania wakicheza pamoja na msanii Ben Pol(mwenye shati nyeupe) kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma usiku wa kuamkia jana.

Msanii Ben Pol akipongezwa na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia jana uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.


Msanii Mimi Mars mdogo wa Vanessa Mdee akifanya yake kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia jana uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Msanii Vanessa Mdee akitoa burudani kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia jana, uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Darassa akitoa burudani kwa maelfu ya wakazi wa Dodoma mapema usiku wa ijumaa

JUX akitoa burudani kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia jana, uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Msanii mkongwe Alli Kiba akiwapa burudani mashabiki wake waliofurika kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia jana uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Thursday, November 2, 2017

ERASTO NYONI MCHEZAJI BORA WA SIMBA OKTOBA

Image result for erasto nyoni
MCHEZAJI Kiraka wa Simba Erasto Nyoni ameibuka mchezaji bora wa klabu hiyo kwa mwezi Oktoba baada ya kuonesha kiwango cha juu katika mechi nne na kuzawadiwa sh 500,000.
Erasto ambaye anamudu kucheza nafasi nyingi uwanjani amekuwa chachu ya matokeo mazuri kwa Simba tangu asajiliwe akitokea Azam FC msimu huu.
Katika taarifa iliyotolewa na SimbaApp inasema katika mwezi Oktoba Simba ilicheza mechi nne na Erasto alicheza vizuri na kuisadiwa timu kupata matokeo mazuri.
“Katika mechi dhidi ya Njombe alichangia upatikanaji wa jumla ya mabao matatu katika mechi hizo nne tangu ligi ianze akiwa ametoa pasi sita za mabao na yeye akifunga moja,” ilisema taarifa hiyo.
Mechi ambazo Erasto alisaidia timu yake ni dhidi ya Stand United, Mtibwa Sugar, Njombe Mji na Yanga ambapo walishinda mechi mbili na kutoka sare mbili.
Kuanzia ligi inaze msimu huu tuzo ya mchezaji bora Agosti ilikwenda kwa mshambuliaji Emanuel Okwi na Septemba ilichukuliwa na kiungo mshambuliaji Mzamiru Yassin.

Simba imeondoka leo kwa ndege kwenda Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bbara dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa kuchezwa Jumapili katika Uwanja wa Sokoine.

SAMATTA KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA

SHIRIKISHO la soka barani Afrika (CAF) limetangaza majina 30 yawachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika huku mtanzania Mbwana Samatta anayecheza KRC Genk ya Ubelgiji akiwa mmoja wapo.
 Licha ya tuzo hiyo CAF pia imewataja wachezaji 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wanaocheza ligi za ndani.
Pamoja na Samatta, wachezaji wengine walioingia kwenye 30 bora ni;
1. Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly)
2. Bertrand Traore (Burkina Faso & Lyon)
3. Cedric Bakambu (DR Congo & Villareal)
4. Christian Atsu (Ghana & Newcastle)
5. Christian Bassogog (Cameroon & Henan Jianye)
6. Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)
7. Eric Bailly (Cote d’Ivoire & Manchester United)
8. Essam El Hadary (Egypt & Al Taawoun)
9. Fabrice Ondoa (Cameroon & Sevilla)
10. Fackson Kapumbu (Zambia & Zesco)
11. Jean Michel Seri (Cote d’Ivoire & Nice)
12. Junior Kabananga (DR Congo & Astana)
13. Karim El Ahmadi (Morocco & Feyenoord)
14. Keita Balde (Senegal & Monaco)
15. Khalid Boutaib (Morocco & Yeni Malatyaspor)
16. Mbwana Samata (Tanzania & Genk)
17. Michael Olunga (Kenya & Girona)
18. Mohamed Salah (Egypt & Liverpool)
19. Moussa Marega (Mali & Porto)
20. Naby Keita (Guinea & RB Leipzig)
21. Percy Tau (South Africa & Mamelodi Sundowns)
22. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)
23. Sadio Mane (Senegal & Liverpool)
24. Thomas Partey (Ghana & Atletico Madrid)
25. Victor Moses (Nigeria & Chelsea)
26. Vincent Aboubakar (Cameroon & Porto)
27. William Troost-Ekong (Nigeria & Bursaspor)
28. Yacine Brahimi (Algeria & Porto)
29. Youssef Msakni (Tunisia & Al Duhail)
30. Yves Bissouma (Mali & Lille)