Monday, September 16, 2013

CLARA BAYO ALIVYO SHINDA TAJI LA REDD'S MISS TANZANIA SPORTS WOMAN 2013


Mrembo Clara Bayo akipunga mkono mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Taji la Redd's Miss Tanzania Sports Woman 2013 wakati wa tamasha la michezo la warembo wanao wania taji la Miss Tanzania 2013. Bayo alifanya vyema katika michezo kadhaa na kujizolea point nyingi na kuwashinda warembo wengine 29. Kwa Taji hilo Clara Bayo ambaye anatoka Kanda ya Ilala, amekuwa mrembo wa nne kuingia nusu fainali za Mashindano hayo makubwa ya urembo nchini ambayo fainali zake zitafanyika Ukumbi wa Mlimani City Septemba 21 mwaka huu.

Clara Bayo akipozi kwa picha.