Friday, November 20, 2015

BENKI YA DTB TANZANIA YAUZA HISA ZENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 30


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Diamond Trust (DTB), Viju Cherian (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Hoteli ya Serena Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu benki hiyo kuuza hisa zenye thamani ya sh. bilioni 30 na kusherehekea miaka 70 ya uwepo wake tangu ianzishwe hapa nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa benki hiyo, Joseph Mabusi.

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa benki hiyo, Joseph Mabusi (kulia), akizungumzia mafanikio mbalimbali na shughuli zinazofanywa na benki hiyo.

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Uzalishaji na Masoko wa benki hiyo, Sylvester Bahati (kushoto), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu masuala mbalimbali ya benki hiyo.

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.