Sunday, November 22, 2015

BUKOBA VETERAN - MASHABIKI WA SIMBA SC WAICHAPA BAO 3-2 MASHABIKI WA YANGA NA KUPATA KOMBE.


Kwa Pamoja Timu na Waamuzi wakiingia Uwanjani tayari kwa kuanza mchezo huo ambao ulichukuwa na sura mbili yaani Mashabiki wa Simba na Mashabiki wa Yanga. Mchezo huo ulichezwa kwenye Uwanja wa Ntungamo Nje kidogo na Mji wa Bukoba.

Wakiingia kwenye Uwanja tayari kwa Mtanange kuchezwa

Wakisalimiana Timu zote mbili, Mchezo huu ni wa maandalizi ya michezo yao miwili ya kirafiki Nchini Uganda Nov 28, 2015 ambapo itacheza Michezo miwili ya kirafiki kati ya  Masaka Veteran na Kampala University.
Wakisalimiana na kutakiana mchezo mwema

Kikosi cha Timu ya Bukoba Veteran ambacho kilicheza Mashabiki wa Timu ya Simba.
Kikosi cha Bukoba Veteran ambacho kilicheza Mashabiki wa Simba SCMc Jerry(kulia) na MwinyiWadau wa Soka
Kipute kikiendelea...
Mashabiki na Wachezaji baadhi wa Timu ya Mashabiki wa Simba wakiwaangalia wenzao
Timu ya Mashabiki wa Simba ndio ilianza kuifunga Timu ya Mashabiki wa Yanga, Mpaka mapumziko walikuwa wanaongoza bao 2-0. Kipindi cha pili dakika ya 49 Timu ya Mashabiki wa Simba walipachika bao la tatu kupitia kwa mchezaji wao Matata Mwakalebela  na kufanya 3-0. Timu ya Mashabiki wa Yanga walizinduka na kupata bao lao la kwanza ambalo walilipata kwa kupewa zawadi kwa mchezaji Shabiki wa  Simba kujifunga kwa kichwa. Bao la pili la Timu ya Mashabiki wa Yanga lilifungwa na Mchezaji wao namba 8 kwa mkwaju wa penati hivyo kufanya mtanange kumalizika kwa dakika 90 kwa Timu ya Mashabiki wa Simba kuibuka Kidedea kwa bao 3-2 na kujinyakulia Kombe. Timu hiyo ya Bukoba Veteran watafanya ziara wiki ijayo Nchini Uganda kucheza Michezo miwili ya Kirafiki na Timu ya Masaka Veteran na Timu ya Chuo cha University. Mtandao wa Bukobasports.com utakuletea live mchezo huo wa kirafiki utaopigwa jumapili Novemba, 2015.

Mwakalebela tena akimiliki mpira..
Patashika kwenye lango Timu ya Mashabiki wa Simba kipa akipangua mpira

Mwakalebela  akifanya yake Uwanjani...kwenye mtanange huo alipachika bao la tatu


Wakiutazama mpira kwa makini...

Wachezaji Mashabiki wa Simba wakishangilia baada ya kuibuka na Ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Mashabiki wa Timu ya Mashabiki wa Yanga Muda mfupi baada ya kipute kumalizika wakiongozwa na (Mwinyi ambaye yupo katikati yao).

Furaha ya Ushindi
Kombe likitolewa kwa Timu Kepteni Kassim ambaye ameiongoza Timu hiyo na kuibuka na UshindiDogo nae Furaha ilimpanda akapandia Kombe juu kwa juu!