Sunday, November 29, 2015

BUKOBA VETERAN WAKUBALI KICHAPO CHA BAO 4-3 KUTOKA KWA WANAFUNZI WA CHUO CHA MUTEESA 1 ROYAL UNIVERSITY, UGANDA

Na Faustine Ruta, Masaka Uganda
Timu ya Bukoba Veteran yenye maskani yake Bukoba Mjini leo hii jumamosi imekubali kichapo cha bao 4-3 kutoka kwa Vijana wa Chuo cha Muteesa 1 Royal University. Mchezo huo wa kirafiki uliopigwa kwenye Mji wa Masaka karibu na Chuo chao kwenye mji wa Masaka Nchini Uganda. Timu hiyo ndio ilianza kuonesha makeke yake kwa kuichapa bao 2-0 Timu ya Bukoba Veteran ndani ya dakika 30 za mwanzo wa kipindi, nayo Bukoba Veteran iliongeza kasi na kuweza kusawazisha bao zote mbili na kujipatia bao la tatu kwa kufanya 3-2. Bao la kusawazisha halikucheleweshwa kabla ya mwamuzi kupiga kipenga kwenda mapumziko timu hizo zilienda mapumziko zikiwa 3-3. Kipindi cha pili dakika ya 90 mchezaji Paul wa Timu ya Chuo cha Muteesa 1 Royal University aliipa bao la ushindi na kuibuka kidedea kwa ushindi wa bao 4-3 dhidi ya timu ya Bukoba Veteran.