Monday, November 23, 2015

FRANCIS COQUELIN NJE MIEZI 2 - ARSENE WENGER

MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger ametamka kuwa Kiungo wao Francis Coquelin atakuwa nje kwa kipindi kisichopungua Miezi Miwili baada ya kuumia Goti Timu yao ilipochapwa 2-1 huko The Hawthorns na West Bromwich Albion.Kipigo hicho cha Jumamosi toka kwa WBA kiliwakosesha Arsenal kukwea kilele cha Ligi Kuu England na kujikuta wametupwa Nafasi ya 4.
Pia kuumia kwa Coquelin na pigo kubwa kuelekea Mwezi Desemba ambao una Mechi mfululizo hadi Mwaka mpya.
Msimu huu, Coquelin, mwenye Miaka 24, ameikamata Namba katika Kikosi cha Kwanza cha Arsenal.

Alipoulizwa ikiwa Kiungo huyo wa Kimataifa wa France ameumia sana, Wenger alijibu: “Siku zote nakuwa mwangalifu lakini nadhani yupo nje si chini ya Miezi Miwili na tunasubiri uchunguzi zaidi.”