Sunday, November 29, 2015

FULL TIME: EIBAR 0 v 2 REAL MADRID, BALE AFUNGA BAO LEO NA KUONDOA UKAME WAKE WA TANGU AUGUST!

Bale akipongezwa kwa bao lake la kwanza kwa Real Bale na Cristiano Ronaldowakipongezana
REAL MADRID, wakiwa Ugenini huko Ipurua Municipal Stadium, wameitandika SD Eibar Bao 2-0 katika Mechi ya La Liga.
Matokeo haya yamewachimbia Real Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Timu ya Pili Atletico Madrid na Vinara Barcelona ambao wako Pointi 5 mbele yao baada ya Mechi 13 za La Liga kwa kila Timu.
Hapo Jana, Barca waliichapa Real Sociedad 4-0 kwa Bao 2 za Neymar na moja moja za Luis Suarez na Lionel Messi.
Atletico waliipiga Espanyol 1-0 kwa Bao la Dakika ya 3 la Antoine Griezmann.
Hii Leo, Real walifunga Bao zao kupitia Gareth Bale, Dakika ya 43, na Penati ya Dakika ya 82 ya Cristiano Ronaldo.

PatashikaVuta nikuvute!