Tuesday, November 17, 2015

KLABU YA MAN UNITED NDIO KINARA KUTOA WACHEZAJI WENGI WA KIMATAIFA ULAYA!

Manchester United ndio inaongoza kwa kutoa Wachezaji wengi wa Kimataifa kwa huko England na pia Barani Ulaya.Msimu huu, Wachezaji wengi wameteuliwa kuzichezea Timu zao za Taifa na Wachezaji wanaocheza Ligi Kuu England ndio wanaongoza kwa Ulaya huku Man United wakiwa juu kwa kutoa Wachezaji wengi zaidi.
Kwa mujibu wa Takwimu za CIES Football Observatory Digital Atlas, Asilimia 41 ya Wachezaji waliocheza Ligi Kuu England Msimu huu wamechezea pia Timu zao za Taifa Msimu huu huu.
Man United wapo juu kwa kutoa Wachezaji Asilimia 72 ya wale walioteuliwa na Meneja wao Louis van Gaal kucheza Mechi za Ligi Kuu England Msimu huu ambao pia waliteuliwa kucheza Timu zao za Taifa.
Ijumaa iliyopita, Wachezaji wa Man United waliovaa Jezi za Nchi zao ni Michael Carrick, Phil Jones, Chris Smalling, Wayne Rooney na Juan Mata ambao walicheza wakati Spain inaichapa England 2-0, wakati Anthony Martial na Morgan Schneiderlin walikuwa kwenye France iliyoichapa Germany ambayo ilikuwa nayo Bastian Schweinsteiger huku Daley Blind akiichezea Netherlands na Matteo Darmian akiichezea Nchi yake Italy.