Tuesday, November 24, 2015

LIGI KUU ENGLAND: CRYSTAL PALACE 0 v 1 SUNDERLAND, DEFOE AIPA USHINDI SUNDERLAND UGENINI! MENEJA SAM ALLARDYCE ACHEKELEA..

Sunderland wamepata ushindi wao wa kwanza wa Ugenini kwenye Ligi Kuu England baada ya Jana Usiku kuifunga Crystal Palace 1-0 huko Selhurst Pak Jijini London.
Bao la ushindi la Sunderland, ambao wako chini ya Meneja maarufu Sam Allardyce aka ‘Big Sam’, lilifungwa Dakika ya 80 na Jermain Defoe aliempora Mpira Scott Dann na kumalizia vizuri.
Ushindi huu umewaweka Sunderland Nafasi ya 18 wakiwa na Pointi 9 kwa Mechi 13 wakati Palace wanabaki Nafasi ya 10 wakiwa na Pointi 19.
Defoe akipeta kulia baada ya kuipa Bao la pekee kwenye mtanange huo uliochezwa Jumatatu usiku dhidi ya Crystal Palace.Yohan Cabaye wa Crystal Palace akiendesha mpira...Meneja wa Zamani wa Newcastle United kwa sasa Crystal PalaceMeneja Sam