Sunday, November 15, 2015

LINGARD AITWA KWA MARA YA KWANZA KIKOSINI ENGLAND, KUIVAA FRANCE JUMANNE KWENYE MECHI YA KIRAFIKI YA KIMATAIFA!

Mchezaji Fowadi wa Manchester United Jesse Lingard ameitwa kwenye Kikosi cha England ambacho kitaivaa France Uwanjani Wembley Jijini London Jumanne Usiku katika Mechi ya Kirafiki.
Lingard, mwenye Miaka 22, amekichezea Kikosi cha Vijana wa England cha U-21 mara 11 lakini hii ni mara ya kwanza kabisa kuitwa kwenye Kikosi cha Kwanza cha England.

Lingard ameitwa Kikosini wakati England ikikabiliwa na Majeruhi baada ya Mchezaji mwenzake wa Man United, Michael Carrick, kuumia walipofungwa Ijumaa na Spain na pia Fowadi wa Leicester, Jamie Vardy, kuwa pia na maumivu na kujiondoa Kikosini.
Lingard alipoingizwa toka Benchi dhidi ya Scotland hapo Agosti 2013 na ni Mchezaji aliekulia Kisoka kwenye Chuo cha Soka cha Man United na kuichezea Timu ya Kwanza yake mara 7 na pia kucheza kwa Mkopo na Klabu za Leicester, Birmingham, Brighton na Derby.

Novemba 7, Lingard aliifungia Man United Bao lake la kwanza wakati wanaifunga West Brom Bao 2-0 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.

KIMATAIFA KIRAFIKI
RATIBA
Jumanne Novemba 17, 2015

3:00 Italy v Poland
3:00 Lebanon v New Zealand
14:00 Macedonia v Lebanon
18:00 Russia v Croatia
19:00 Estonia v Saint Kitts And Nevis
19:00 Azerbaijan v Moldova
20:15 Turkey v Greece
21:30 Luxembourg v Portugal
21:45 Austria v Switzerland
21:45 Poland v Czech Republic
21:45 Slovakia v Iceland
21:45 Belgium v Spain
22:00 England v France
22:45 Germany v Netherlands
22:45 Italy v Romania