Thursday, November 19, 2015

LIONEL MESSI ACHEKELEA MECHI YA EL CLASICO YA JUMAMOSI, ASEMA LAZIMA MTU AKAE!

Viongozi wa Spain wakiahidi ulinzi mkali Jumamosi Uwanjani Santiago Bernabeu kwenye ule mtanange mkali kati ya Miamba ya La Liga Mabingwa Barcelona na Real Madrid unaobatizwa 'El Clasico', stori ya mjini ni kitendawili kama Supastaa Lionel Messi ataanza Mechi hii.
Ulinzi mkali umeahidiwa huko Bernabeu kufuatia hali tete ya usalama huko Ulaya iliyosababisha Mechi kubwa kadhaa kufutwa kutokana na vitisho kufuatia mauaji mabaya ya Watu 129 huko Paris Ijumaa iliyopita.

Jumamosi, ndani ya Bernabeu, kunatarajiwa kuwa na Washabiki 80,000 Vitini wakilindwa na Polisi na Wanausalama wengine idadi yao ikiwa maradufu ya ile ya kawaida.
Kisoka, Mechi hii, mbali ya kuwa ni El Clasico, safari hii inawakutanisha Barcelona, wanaaoongoza La Liga wakiwa Pointi 3 mbele, na Real Madrid walio Nafasi ya Pili.
Lakini mvuto mkubwa Siku zote ni ile vita binafsi kati ya Mastaa wa Klabu hizi mbili, Cristiano Ronaldo wa Real na Messi wa Barca.
Wakati Ronaldo yuko fiti na alipumzishwa na Nchi yake Portugal kucheza Mechi za Kimataifa wakati Ligi imesimama kwa Wiki 2 huku mwenyewe akijifua kivyake, Messi alikuwa nje ya Uwanja tangu Septemba 28 alipoumia Goti.
Lakini, kwa takriban Wiki moja sasa, Messi anerejea Mazoezini na swali ni je Kocha wa Barca, Luis Enrique, atamuanzisha Mechi hii?