Sunday, November 22, 2015

TOTTENHAM HOTSPUR 4 v 1 WEST HAM UNITED

Tottenham Leo wamepaa hadi Nafasi ya 5 katika Ligi Kuu England baada ya kuitandika West Ham Bao 4-1 Uwanjani White Hart Lane.
Ushindi huu umewafanya Spurs wawe hawajafungwa katika Mechi 12 za Ligi na kuifikia rekodi yao wenyewe kutofungwa katika Mechi nyingi za Ligi.
Hadi Mapumziko Spurs waliongoza 2-0 kwa Bao za Harry Kane na Toby Alderweireld.
Kipindi cha Pili akapiga Bao la 3 na Kyle Walker kuipa Spurs uongozi wa Bao 4-0.
Zikisalia Dakika 3, Manuel Lanzini akaipa West Ham Bao la kufutia machozi.
Timu hizi zilianza Mechi hii zote zikiwa na Pointi 21 kwa Mechi 12 na ushindi huu umewapaisha Tottenham na kushika Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Timu ya 4 Arsenal.
Mechi ifuatayo ya Ligi kwa Tottenham ni dhidi ya Mabingwa Chelsea.

VIKOSI:
Tottenham Hotspur:
Lloris, Walker, Alderweireld, Vertonghen, Rose, Dier, Alli, Son, Dembele, Eriksen, Kane
Akiba: Mason, Vorm, Trippier, Townsend, Onomah, Carroll, Davies.
West Ham United: Adrian, Jenkinson, Tomkins, Reid, Cresswell, Kouyate, Noble, Moses, Lanzini, Sakho, Carroll
Akiba: Song, Zarate, Ogbonna, Jelavic, Antonio, Spiegel, Oxford.
REFA: Anthony Taylor