Friday, November 13, 2015

MANCHESTER UNITED MAPATO YA ROBO YA KWANZA YA MWAKA HAISHIKIKI, KUWEKA REKODI YA KIHISTORIA!

Manchester United wametangaza Mapato yao ya Robo ya Kwanza ya Mwaka wa Kifedha na wako mbioni kuvunja kile kihunzi cha kuvuka Mapato ya Pauni Milioni 500 kwa Klabu na kuweka Rekodi ambayo hajafikiwa na Klabu yeyote.
Mapato ya Man United kwa Miezi Mitatu, iliyoiishia Septemba, ni Pauni Milioni 123.6 ikiwa ni ongezeko la Asilimia 39 kwa kipindi kama hiki kwa Mwaka 2014.

Mapato ya Man United yamepata kiki baada ya kusaini Mkataba mpya na Adidas ambayo yatawaingizia Pauni Milioni 750 kwa Miaka 10 ukiwa ni Mkataba mkubwa kabisa Duniani kwa Klabu na Watengeneza Vifaa vya Michezo.
Vilevile, kurudi kwa Man United kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI kumechangia ongezeko la pato lao kwenye Matangazo ya Mechi kwa Asilimia 64.3 na pia kwa Asilimia 64.2 kwa Siku za Mechi kutokana na Viingilio na bidhaa nyingine wakati wa Mechi.