Saturday, November 7, 2015

MANCHESTER UNITED 2-0 WEST BROM ALBION, JUAN MATA NA JESSE LINGARD WAIPA USHINDI UNITED OLD TRAFFORD LEO


Bao za Kipindi cha Pili za Jesse Lingard na Juan Mata Leo zimewapa Manchester United ushindi wa Bao 2-0 walipocheza na West Bromwich Albion kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Uwanjani Old Trafford.
Mapema Kipindi cha Pili, Lingard, mwenye Miaka 22, aliifungia Man United Bao la Kwanza kwa shuti la kupinda na Juan Mata kuongeza Bao la Pili katika Dakika za Majeruhi kwa Penati baada ya Anthony Martial kuchezewa Faulo na Gareth McAuley ambae alitolewa kwa Kadi Nyekundu.Ushindi huu umewabakisha Man United Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England ikiwa ni ushindi wao wa kwanza baada ya Mechi 3 za Ligi na Mechi yao inayofuata ni ugenini na Watford hapo Novemba 21.
Mata akichonga penatiBastian ChiniCameron nae leo kacheza na Timu ya wakubwaLingard akipongezwaJesse akiponngezwa kwa bao safiJesse akishangiliaDe Gea nae alifurahia baoShangwe!Martial akichuana na EvansWakiunga UkutaWanajuana: Rooney na Fletcher