Thursday, November 19, 2015

MARTIAL AZUA JAMBO OLD TRAFFORD!

Anthony Martial ameipa Manchester United wasiwasi mkubwa baada ya kuondoka Uwanjani Wembley Jana Usiku akitembelea Magongo.
Martial, mwenye Miaka 19, Jana aliichezea France ilipofungwa 2-0 na England katika Mechi ya Kirafiki na kuumia Mguu wake wa Kushoto na kutolewa nje katika Dakika ya 67.
Wakati akiondoka Wembley baada ya Mechi hiyo Mguu wa Kushoto wa Straika huyo ulifungwa Bendeji nzito na alikuwa akitembea kwa msaada wa Magongo.

Hali hii itampa wasiwasi mkubwa Meneja wa Man United Louis van Gaal ambae anamtegemea sana Chipukizi huyo aliefunga Bao 5 tangu ahamie hapo Septemba 1 akitokea AS Monaco ya France.
Kocha wa France, Didier Deschamps, ameeleza Martial aliumia juu ya Mguu karibu na Vidole.
Huyu ni Mchezaji wa Pili wa Man United kuumia katika Wiki hii ya Mechi za Kimataifa baada ya Kiungo Michael Carrick kuumia Ijumaa iliyopita akiichezea England ilipofungwa 2-0 na Spain huko Alicante.
Jumamosi Man United inacheza Ugenini na Watford kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Ni shida Martial akiondoka Wembley kwa Magongo!