Saturday, November 14, 2015

MATUKIO YA MECHI SPESHO OLD TRAFFORD LEO! GREAT BRITAIN & IRELAND 3-1 REST OF THE WORLD...SIR ALEX FERGUSON ASHINDA TENA OLD TRAFFORD!

Paul Scholes akipongezwa baada ya kufunga bao la kwanza..
Mechi Spesho ya UNICEF ambayo imeratibiwa na David Beckham ili kusaidia Watoto katika Nchi 190 za Dunia imeisha kwa Timu ya Uingereza & Ireland kuipiga Timu ya Dunia Bao 3-1 Uwanjani Old Trafford mbele ya Mashabiki 75,381.
Beckham, ambae ni Balozi wa UNICEF kwa Miaka 10 sasa, ndie aliebuni wazo la kucheza Mechi hii kuchangisha Fedha, na ni yeye aliesababisha Bao la kwanza baada ya Krosi yake kuunganishwa kwa Kichwa na Paul Scholes na kuipa Uingereza & Ireland, chini ya Meneja Sir Alex Ferguson, uongozi wa 1-0 hadi Haftaimu


Timu ya Dunia ilikuwa chini ya Meneja Carlo Ancelotti na Kepteni Luis Figo ambae alichukua wadhifa huo baada ya Zinedine Zidane kujitoa kutokana na maafa huko kwao France na ni Dwight Yorke aliewapa Bao lao 1 huku Michael Owen akifunga Bao nyingine 2 kwa Uingereza & Ireland.

Kivutio kikubwa kwa Mechi hii ni pale David Beckham alipotoka nje ya Uwanja na Mwanawe, Brooklyn, mwenye Miaka 16, kuingia badala yake katika Dakika ya 75.
Timu ya Uingereza & Ireland imeibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Timu ya Dunia.

Darren FletcherDavid Becham Luis Figo na Ryan GiggsTimu ya Uingereza & Ireland imekuwa chini ya Meneja Sir Alex FergusonMeneja Sir Alex FergusonWakiwa kwenye picha ya pamoja na WatotoMechi maalum ya David Beckham kwa WatotoTimu ya Uingereza & Ireland imeibuka na ushindi wa bao 3-1 dhidi ya Timu ya Dunia. Wanasoka wakongwe Taswira kamili ya Vikosi kabla ya Mtanange kuanza kwenye Uwanja wa Old Trafford leoDaavid Beckham kabla ya mtanange leo hii jioniSir Alex Ferguson na Carlo Ancelotti 
Wakiingia Uwanjani tayari kwa kipute..kuanza
VIKOSI:
Great Britain & Ireland:
James, Carragher, Terry, A Cole, P Neville, Beckham (Kepteni), Butt, Fletcher, Giggs, Scholes, Crouch
Akiba: Seaman, Campbell, Sinclair, McAllister, Smith, Owen
Magoli: Scholes, Dakika ya 14, Owen 63, 85
Meneja: Sir Alex Ferguson

Timu ya Dunia: Van Der Sar, Cafu, Couto, Silvestre, Figo (Kepteni), Seedorf, Pires, Park, Ronaldinho, Kluivert, Solskjaer
Akiba: Van der Gouw, Hierro, Donovan, Yorke
Goli: Yorke, Dakika ya 67
Meneja: Carlo Ancelotti
Marefa: Pierluigi Collina, Anthony Taylor