Monday, November 9, 2015

VAN GAAL ATOBOA KUWA BAADHI YA CHIPUKIZI WAKE KUCHEZA KATIKA KIKOSI CHA KWANZA..MAN UNITED.

BOSI wa Manchester United ameeleza Chipukizi wengi wa Klabu yao watapata fursa za kuwemo Kikosi cha Kwanza baada ya Jumamosi Cameron Borthwick-Jackson kucheza kwa mara ya kwanza wakati Man United inaifunga West Brom 2-0.
Kwa Mechi mbili sasa, Chipukizi Axel Tuanzebe, mwenye Miaka 17 na ni Mzaliwa wa Congo DR ambae pia ana Uraia wa Uingereza na Cameron Borthwick-Jackson, mwenye Miaka 18, walikuwemo kwenye Mechi za Ligi Kuu England dhidi ya Crystal Palace na West Brom.
Kwenye Mechi na West Brom, Cameron Borthwick-Jackson aliingizwa katika Dakika ya 77 kumbadili Marcos Rojo na kucheza vizuri tu.
Wawili hao wanafuata nyayo za Jesse Lingard na Paddy McNair ambao wamepanda kutoka Timu za Vijana hadi kuwemo kwenye Kikosi cha Timu ya Kwanza.
Van Gaal ameeleza falsafa yake ni kuwapa Vijana nafasi kucheza Timu ya Kwanza.
Van Gaal amesema: “Hivi ndivyo ninavyoongoza Timu. Sitaki Wachezaji wengi kwani Vijana watakosa fursa. Ndio Maana nimeuza Wachezaji wengi na wengi wako nje kwa Mkopo. Sasa tunao Wachezaji 21 na Makipa Watatu.”
Aliongeza: “Ikitokea tuna Majeruhi au Ugonjwa, natizama Timu za Vijana na Makocha wangu wa Timu hizo Warren Joyce na Paul McGuinness. Mara ya mwisho nilimchukua Tuanzebe kwa sababu Phil Jones alikuwa mgonjwa. Nikamchukua Borthwick-Jackson kwa sababu Rojo amecheza Mechi mfululizo.”