Friday, November 20, 2015

WAYNE ROONEY, MARTIAL, FELLAINI KUIKOSA WATFORD KESHO!

MENEJA Louis van Gaal Leo amethibitisha kuwa Wachezaji wake mahiri Wayne Rooney na Anthony Martial wataikosa Mechi ya Manchester United ya Ugenini Jumamosi huko Vicarage Road dhidi ya Watford katika Ligi Kuu England.
Wakati Kepteni Wayne Rooney ni mgonjwa, Martial anaungana na Majeruhi wengine Michael Carrick, Marouane Fellaini, Antonio Valencia na wa muda mrefu Luke Shaw.

Kukosekana kwa Rooney, Martial na Fellaini kunampa wakati mgumu Van Gaal wa kumpata Sentafowadi kwani aliebaki ni Chipukizi James Wilson ambae nae ndio kwanza tu amepona maumivu na kuanza mazoezi na hivyo hataweza kucheza Dakika zote 90.
Chaguo lilobaki ni Memphis Deepay na Jesse Lingard lakini nae Deepay hajaanza Mechi ya Ligi tangu Oktoba 4 Man United ilipofungwa 3-0 huko Emirates na Arsenal.
Hata hivyo, habari njema kwa Man United ni kuwa Rooney na Martial wote wanatarajiwa kuwa fiti kwa Mechi ijayo ya UEFA CHAMPIONS LIGI dhidi ya PSV Eindhoven itakayochezwa Wiki ijayo Uwanjani Old Trafford.
Fellaini.