Friday, November 20, 2015

WAZIRI MKUU WA 11 KASSIM MAJALIWA, NAIBU SPIKA NI DK. TULIA

Waziri Mkuu Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa, akitoka kwenye ukumbi wa bunge mjini dodoma jana mara baada ya kuthibitishwa uteuzi wake na bunge. (Picha na Said
Waziri Mukuu Mteule, Majaliwa Kassim Majaliwa, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuteuliwa na kuthibitishwa na bunge mjini Dodoma jana, ambapo anatarajiwa kuapishwa leo Ikulu ya Chamwino.
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola, akichangia hoja ya uteuzi wa jina la Waziri Mkuu bungeni mjini Dodoma jana, ambapo alichafua hali ya hewa aada ya kuwataja wabunge wawili wa upinzani kuwa wamefurahia uteuzi huo.
Waziri Mkuu Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa. Waziri Mkuu Mteule akiwashukuru wabunge mara baada ya kumthibitisha.
Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson, akiapa kiapo cha utii mara baada ya kuchaguliwa na wabunge kwenye nafai hiyo mjini Dodoma.
Wabunge wa CCM wakishangilia kumpongeza Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Ackson (wanne kulia) nje ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma.