Sunday, December 27, 2015

ARSENE WENGER ALILIA KIPIGO CHA BAO 4-0 WALICHOSHUSHIWA NA SOUTHAMPTON! AJITETEA KWA KUMWANGUSHIA LAWAMA REFA JONATHAN MOSS!

Baada ya Jana Arsenal kutandikwa 4-0 huko Uwanja wa Mtakatifu Maria na Southampton, maarufu kama Watakatifu, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, alilalamika kuhusu kipondo hicho.
Wenger alielezea sababu zilizowafungisha na lawama kubwa kumshukia Refa Jonathan Moss kwa kipigo hicho kilichowakosesha nafasi murua kutua kileleni mwa Ligi Kuu England.
Wenger alieleza: "Tulipoteza nafasi nyingi za kukaba na kumiliki tena Mipira na hilo lilitugharimu na kupoteza Gemu. Hilo ni upande mmoja na nawasifu Southampton kwa kukaba vizuri wakitumia miguvu."

"Kitu cha pili ni kuwa katika Goli 3 za kwanza tulikosa bahati ya maamuzi ya Refa. Goli la kwanza ni Ofsaidi, Goli la pili ni faulo na la 3 ni Golikiki. Ukicheza chini ya kiwango na juu yake Goli 3 za utata ni ngumu!"