Monday, December 21, 2015

BOSI RAYO VALLECANO ADAI KIPIGO CHA 10-2 TOKA KWA REAL NI FEDHEHA NA KUZALILISHWA NA AIBU KWA ‘LIGI BORA DUNIANI’!

BOSI wa Rayo Vallecano Paco Jemez amesema Timu yake ilifedheheshwa na kudhalilishwa ilipobamizwa Mabao 10-2 hapo Jana kwenye Mechi ya La Liga Uwanjani Santiago Bernabeu.
Bao za Real kwenye Mechi hiyo zilifungwa na Gareth Bale, Bao 4, Karika Benzema, Bao 3, Cristiano Ronaldo, 2 na Danilo Bao 1.
Jimenez kipigo hicho kimeaibisha Soka la Spain na kuipotezea imani.
Amedai: “Tumefedheheka na kudhalilihwa. Hii haisaidia Real, au sisi, au Soka la Spain. Leo, hakuna alieshinda. Sote tumepoteza. Ni aibu, ni fedheha. Kuna vitu vinatokea na natumai sitaviona tena!”
Kwenye Mechi hiyo, Rayo Vallecano walitangulia 2-1 lakini walipigwa na dhoruba baada ya Wachezaji wao Wawili kutolewa kwa Kadi Nyekundu ndani ya Nusu Saa ya kwanza.

Jimenez ameeleza: “Ni muda mrefu sijaona mambo ya kustaajabisha kama haya, yanatia aibu. Siwezi kueleza Zaidi, anaetaka kuelewa ataelewa tu! Hii inawezaje kutokea katika Ligi Bora Duniani? Haipaswi kutokea kokote kule!” Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Real Madrid kufunga Bao 10 kwenye Mechi ya La Liga tangu Mwaka 1960 walipoifunga Elche 11-2.
Akijibu madai ya Jimenez, Kocha wa Real, Rafa Benitez, alisema: "Kuna Gemu nyingi hata sisi tulionewa, hatukunufaika. Sikusema lolote wakati huo na sitasema kitu sasa.”
La Liga sasa inaenda Mapumziko ya Siku 10 kwa ajili ya Krismasi na Mwaka mpya.
Bale!