Wednesday, December 2, 2015

CAPITAL ONE CUP: EVERTON, STOKE, MAN CITY WASHINDA...WATANGULIA NUSU FAINALI!

TIMU za Ligi Kuu England, Everton, Stoke na Man City Leo zimeingia Nusu Fainali za Kombe la Ligi huko England, ambalo hujulikana kama Capital One Cup, baada ya kushinda Mechi zao za Robo Fainali dhidi ya Timu za Madaraja ya chini.
Wakiwa kwao Etihad, Man City waliichapa Hull City Bao 4-1 baada ya kuongoza 4-0 kwa Bao za Wilfied Bony, Kelechi Iheanacho na Bao 2 za Kevin De Bruyne na Hull kupata Bao lao moja Dakika za mwishoni kupitia Andrew Robertson.
Everton, wakicheza Ugenini huko Riverside Stadium, waliifunga Middlesbrough Bao 2-0 kwa Bao za Kipindi cha Kwanza za Gerard Deulofeu na Romelu Lukaku.
Nako huko Britannia Stadium, Stoke City waliipiga Sheffield Wednesday Bao 2-0 kwa Bao zilizofungwa na Ibrahim Afellay na Phil Bardsley.

Hii ni mara ya kwanza kwa Stoke kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Ligi tangu Mwaka 1972 walipotwaa Kombe hili.
Kesho ipo Mechi ya mwisho ya Robo Fainali ya Kombe hili wakati Timu za Ligi Kuu England pekee zitakapocheza na ni kati ya Southampton na Liverpool.

Capital One Cup
Robo Fainali
MATOKEO
Jumanne Desemba 1

Middlesbrough 0 vs  Everton 2
Stoke City 2 vs Sheffield Wednesday 0
Manchester City 4 vs Hull City 1

Capital One Cup
Robo Fainali
Mechi kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
Jumatano Desemba 2

Southampton vs Liverpool