Sunday, December 13, 2015

CLUB WORLD CUP: SANFRECCE HIROSHIMA WAWAKARIBISHA KWA KICHAPO TP MAZEMBE CHA BAO 3-0.


Baadhi ya Wachezaji wa Timu ya Sanfrecce Hiroshima wakipongezana baada ya kuwanyuka Mabingwa wa Africa TP Mazembe bao 3-0 leo kwenye Mchezo wa Club World Cup.

WENYEJI wa Mashindo ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu, Sanfrecce Hiroshima ya Japan, Leo wamewatandika Mabingwa wa Afrika TP Mazembe ya Congo DRBao 3-0 na kutinga Nusu Fainali.

Bao za Hiroshima zilifungwa na Tsukasa Shiotani, Dakika ya 44, Kazuhiko Chiba, 56, na Takuma Asano, 78.
Kwenye Nusu Fainali Hiroshima watakutana na River Plate inayoanzia hatua hiyo.
Nao TP Mazembe wao watacheza na America, ambayo mapema Leo, ilichapwa 2-1 Guangzhou Evergrande, ili kusaka Mshindi wa 5.
Kwenye Nusu Fainali, Guangzhou Evergrande itacheza na Barcelona wanaoanzia Nusu Fainali.


Klabu zinazoshiriki:
-River Palate [Argentina]: Mabingwa wa Copa Libertadores
-Barcelona [Spain]: Mabingwa wa Ulaya
-Guangzhou Evergrande [China]: Mabigwa wa Asia
-TP Mazembe [Congo DR]: Mabingwa wa Afrika
-America [Mexico]: Mabingwa wa CONCACAF
-Auckland City [New Zealand]: Mabingwa wa Oceania
-Sanfrecce Hiroshima [Japan]: Wenyeji-Ni Mabingwa wa Japan

FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU
Ratiba/Matokeo:

Raundi ya Awali
10 Desemba 2015
Sanfrecce Hiroshima 2 Auckland City 0
Robo Fainali
13 Desemba 2015
América 1 Guangzhou Evergrande 2 [Mechi Na. 2]
Nagai Stadium, Osaka
13 Desemba 2015
TP Mazembe 0 Sanfrecce Hiroshima 3 [Mechi Na. 3]
Nagai Stadium, Osaka
Mshindi wa 5
16 Desemba 2015
10:30
América v TP Mazembe
Nagai Stadium, Osaka
Nusu Fainali
16 Desemba 2015
13:30

Sanfrecce Hiroshima v River Plate
Nagai Stadium, Osaka
17 Desemba 2015
13:30
Barcelona v Guangzhou Evergrande
International Stadium Yokohama, Yokohama
Mshindi wa 3
20 Desemba 2015

10:00
International Stadium Yokohama, Yokohama
Fainali
20 Desemba 2015

13:30
International Stadium Yokohama, Yokohama