Saturday, December 12, 2015

DROO YA EURO 2016 YAFANYIKA LEO! ENGLAND KUPAMBANA NA WALES KUNDI B, RUSSIA NA SLOVAKIA KUPAMBANA WAKIWA KWENYE KUNDI HILO KIFO!

DROO ya kupanga ya kupanga Makundi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, imefanyika Leo huko Paris Nchini France ambako Fainali hizo zitafanyika.
Fainali hizo zitakuwa na Timu 24 ambazo zimegawanywa katika katika Makundi 6 ya Timu 4 kila moja.
Wenyeji France wako Kundi A pamoja na Albania, Romania na Switzerland.
France watafungua dimba Mashindano hayo kwa kucheza na Romania.
Fainali za EURO 2016 zitachezwa Mwakani kuanzia Juni 10 hadi Julai 10 huko France.

MAKUNDI:
KUNDI A: France, Romania, Albania, Switzerland.
KUNDI B: England, Russia, Wales, Slovakia.
KUNDI C: Germany, Ukraine, Poland, Northern Ireland.
KUNDI D: Spain, Turkey, Czech Republic, Croatia.
KUNDI E: Belgium, Republic of Ireland, Sweden, Italy.
KUNDI F: Portugal, Iceland, Austria, Hungary.

Fainali zitafanyika lini:
Euro 2016 itaanza Ijumaa Juni 10 na kumalizika Jumapili Julai 10.
Hii ni mara ya kwanza kwa Fainali hizi kuwa na Timu 24 na hivyo itakuwepo Raundi ya Mtoano ya Timu 16, kisha Robo Fainali na Nusu Fainali.

Viwanja vya Mechi za Fainali:
Euro 2016 itatumia Viwanja 10 Nchini France:
Stade de Bordeaux, Bordeaux (Watu 42,000)
Stade Bollaert Delelis, Lens Agglo (35,000)
Stade Pierre Mauroy, Lille Metropole (50,100)
Stade de Lyon, Lyon (58,000)

Stade Velodrome, Marseilles (67,000)
Stade de Nice, Nice (35,000)
Parc des Princes, Paris (45,000)
Stade de France, Saint-Denis (80,000)
Stade Geoffroy Guichard, Saint-Etienne (41,500)
Stadium de Toulouse, Toulouse (33,000)
 
Fainali itachezwa Stade de France