Monday, December 14, 2015

DROO YA EUROPA LEAGUE NAYO LEO! MAN UNITED, LIVERPOOL, SPURS KUPATA WAPINZANIA WAO RAUNDI YA MTOANO TIMU 32!

www.bukobasports.comLEO huko Nyon, Uswisi, UEFA EUROPA LIGI inafanya Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 kwa kujumuisha Timu 24 zilizofuzu kutoka Makundi ya Mashindano haya na Timu 8 zilizomaliza Nafasi za 3 kwenye Makundi ya UEFA CHAMPIONS LIGI mojawapo ikiwa Manchester United.
Pamoja na Man United kwenye Droo hiyo zipo pia Liverpool na Tottenham ambao walifuzu kutoka Makundi ya EUROPA LIGI.
Timu 8 zilizotoka UEFA CHAMPIONS LIGI ni Man United, Bayer Leverkusen, Olympiacos, Porto, Shakhtar Donetsk, Galatasaray, Sevilla na Valencia.
Kwenye Droo, Timu hizo 32 zimegawanywa kwenye Vyungu Viwili vya Timu 12 kila kimoja huku Chungu Namba 1 kikiwa na Timu zilimaliza Washindi wa Makundi yao pamoja na zile ambazo ziko juu kwenye Listi ya Ubora ya UEFA.
Timu iliyo Chungu Namba 1 itapangwa kucheza na Timu iliyo Chungu Namba 2 isipokuwa Timu za Nchi moja hazitakutanishwa na zile zilizokuwa Kundi moja hazitapangwa kukutana.
Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 zitachezwa Februari 18 na Marudiano ni Februari 25.

DROO-Vyungu-Raundi ya Mtoano ya Timu 32:
Chungu Namba 1:

Molde, Liverpool, Krasnodar, Napoli, Rapid Wien, Braga, Lazio, Lokomotiv Moskva, Basel, Tottenham Hotspur, Schalke, Athletic Club, Manchester United*, Bayer Leverkusen*, Olympiacos*, Porto*

Chungu Namba 2: 

Fenerbahçe, Sion, Borussia Dortmund, Midtjylland, Villarreal, Marseille, St-Étienne, Sporting CP, Fiorentina, Anderlecht, Sparta Praha, Augsburg, Shakhtar Donetsk*, Galatasaray*, Sevilla*, Valencia*