Thursday, December 3, 2015

FIFA LISTI YA UBORA DUNIANI: BELGIUM BADO NI NAMBARI 1, TANZANIA YAPANDA 3 NI YA 132!

Belgium imebaki Nambari Wani kwenye FIFA Listi ya Ubora Duniani iliyotolewa Leo huku Tanzania ikipanda Nafasi 3.
Mabingwa wa Dunia Germany wameshuka Nafasi 2 na sasa wapo Nafasi ya 4 wakati Argentina wakipinda Nafasi 1 na kushika Nafasi ya Pili na Spain kupanda Nafasi 3 na kukamata Nafasi ya 3.
Brazil nao wapo Nafasi ya 6 baada kupanda Nafasi 2.
Tanzania sasa ipo Nafasi ya 132 baada ya kupanda Nafasi 3 toka Mwezi uliopita.
Kwa Afrika, Timu ya juu kabisa kwenye Listi ya Ubora ni Ivory Coast ambayo ipo Nafasi ya 19 baada ya kupanda Nafasi ikifuatiwa na Algeria ambayo ipo Nafasi ya 28 baada ya kuporomoka Nafasi 2.

10 BORA:
1. Belgium
2. Argentina
3. Spain
4. Germany
5. Chile
6. Brazil
7. Portugal
8. Colombia
9. England

10. Austria