Saturday, December 12, 2015

FULL TIME: BARCELONA 2 v 2 DEPORTIVO LA CORUNA


NOU CAMP Leo iligeuka kutoka chereko na kuwa huzuni baada ya Vinara wa La Liga kuongoza 2-0 hadi Dakika ya 77 na kuiruhusu Deportivo La Coruna kuambua Sare ya 2-2.

Licha ya matokeo haya Barca, ambao ndio Mabingwa Watetezi, bado wapo kileleni wakiwa na Pointi 37 baada ya Mechi 15 wakifuatiwa na Atletico Madrid wenye Pointi 32 kwa Mechi 14 na Real Madrid Pointi 30 kwa Mechi 14.

Barca waliongoza 1-0 hadi Mapumziko kwa Frikiki safi ya Lionel Messi ya Dakika ya 39 na Ivan Rakitic kupiga Bao la Pili Dakika ya 62 kwa mzinga mkali.

Deportivo La Coruna walizinduka na kufunga Bao zao Dakika za 77 kupitia Martinez Lucas Perez na Dakika 86 kwa Bao la Alex Bergantinos.

VIKOSI:
Barcelona: 13-Bravo, 6-Dani Alves, 3-Piqué, 14-Mascherano, 18-Alba, 4-Rakitic, 5-Busquets, 8-Iniesta, 10-Messi, 09-Suárez, 19-Ramírez

Akiba: 1-Ter Stegen, 15-Bartra, 17-Munir, 20-S Roberto, 21-Adriano, 23-Vermaelen, 24-Mathieu.

Deportivo La Coruna: 1-Lux, 15-Sanabria Ruiz, 14-Arribas, 12 da Silva Junior, 3-Navarro Corbacho, 11-Juanfran, 4-Bergantiños García, 19-Fajr, 16-Correia Pinto, 20-Rodríguez Portillo, 7-Pérez Martínez

Akiba: 25-Manu Fernandez, 6-Cani, 8-Medunjanin, 10-Juan Dominguez, 21-Luis Alberto, 23-Lopo, 30-Cardoso.