Wednesday, December 2, 2015

KWA NINI MASHABIKI WALIOWENGI WA MAN UNITED HAWANA FURAHA?

Man United wako nafasi ya tatu na pamoja na hayo wako ndani ya Top 4 na wakiongeza bidii waweza kupaa kileleni siku za usoni lakini Mashabiki wake walio wengi hawana furaha kwa kile kinachoonekana kucheza kwake. Wanaona klabu hiyo inacheza kwa kulinda kuliko kushambulia na kufunga mabao.