Monday, December 14, 2015

LA LIGA: REAL YATUNGULIWA BAO 1-0 NA VILLARREAL, ATLETICO YAIKAMATA BARCELONA KILELENI!


Real Madrid wamefungwa 1-0 na Villarreal na kujikuta wako Pointi 5 nyuma ya Vinara wa La Liga Barcelona na Atletico Madrid ambao Jana waliifunga Athletic Bilbao 2-1 kuikamata Barca kileleni kwa Pointi.
Bao la ushindi la Villareal lilifungwa na Roberto Soldado Dakika ya 8 tu ya Kipindi cha Kwanza walichotawala chote na Kipindi cha Pili kujihami vyema baada ya Real kucharuka.
Real sasa wako Nafasi ya 3 kwenye La Liga wakiwa Pointi 2 tu juu ya Timu ya 4 Celta Vigo na Pointi 3 mbele ya Timu ya 5 Villareal.
Kipigo hiki kinaleta presha kubwa kwa Meneja wa Real, Rafa Benitez, baada ya kuchapwa 4-0 na Barcelona kwenye El Clasico na pia kutupwa nje ya Copa del Rey kwa kumchezesha Meneja asiestahili.Huko Vicente Calderon, Atletico Madrid wameinasa Barcelona kileleni baada ya Bao za Saul Ñíguez na Antoine Griezmann kuwapa ushindi wa 2-1 Athletic Bilbao.
Juzi, Barca waliongoza 2-0 na kujikuta wakitoka Sare na Deportivo La Coruna.

LA LIGA
Matokeo:
Jumamosi Desemba 12

FC Barcelona 2 v Deportivo La Coruna 1
Celta de Vigo 1 v RCD Espanyol 0
Levante 1 v Granada 2
Sevilla FC 2 v Sporting Gijon 0
Las Palmas 1 v Real Betis 0
Jumapili Desemba 13
Rayo Vallecano 1 v Malaga 2
SD Eibar 1 v Valencia C.F 1
Atletico de Madrid 2 v Athletic de Bilbao 1
Villarreal CF 1 v  Real Madrid 0