Monday, December 28, 2015

LEO MAN UNITED v CHELSEA, NANI KUIBUKA KIDEDEA OLD TRAFFORD?

DAIMA Manchester United na Chelsea zikikutana kwenye Ligi Kuu England kila Mdau hukodolea macho mtanange huu kwani mara nyingi moja au Timu zote huwa Mdau mkubwa katika mbio za Ubingwa lakini safari hii hali ni tofauti kabisa.Wakati Chelsea ndio Mabingwa Watetezi, Msimu wao ulisambaratika kitambo kwani sasa wako Nafasi ya 15 wakiwa Pointi 19 nyuma ya Vinara Leicester City na leo  Jumatatu Usiku ndio wanacheza Mechi yao ya 19 ikiwa ni nusu ya Mechi zao zote za Ligi kwa Msimu huu. Ukilinganisha  Chelsea, Man United wana ahueni kidogo kwani wako Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 10 mbele ya Chelsea lakini wanatinga kwenye Mechi hii Uwanjani kwao Old Trafford wakiwa wamefungwa Mechi 4 mfululizo, 3 zikiwa za Ligi, na hali hii sasa imetoa presha na uvumi mkubwa wa kufukuzwa kwa Meneja wao Louis van Gaal ambae inadaiwa kuwa matokeo mabovu kwenye Mechi hii basi hana chake.
LEO Jumatatu Usiku, kwenye Mechi hii ya mwisho kabisa kwa Mwaka 2015 kwa kila Timu, Van Gaal anakutana na Mdachi mwenzake Guus Hiddink ambae hii ni Mechi yake ya Pili baada ya Jumamosi kuanza kwa Sare ya 2-2 na Watford akiwa amechukua wadhifa kutoka kwa Jose Mourinho alietimuliwa Wiki iliyopita.

DONDOO MUHIMU:
-Man United haijaifunga Chelsea katika Mechi 8 zilizopita [Kufungwa 5 Sare 3]
-Ikiwa Man United watafungwa Mechi hii, hii itakuwa mara ya kwanza tangu 1936 kufungwa Mechi 5 mfululizo. Mara ya mwisho kufungwa Mechi 4 mfululizo ni Msimu wa 1961/62
Hali za Wachezaji
Kepteni wa Man United Wayne Rooney huenda akaanza Mechi hii baada ya kuanzia benchi walipofungwa na Stoke na pia Kiungo Bastian Schweinsteiger anaweza kucheza baada ya kumaliza Kifungo chake cha Mechi 3.

Pia, Man United safari hii wanaweza kumtumia Winga Ashley Young kama Winga badala ya Fulbeki wa Kulia baada ya kupona kwa Matteo Darmian.
Chelsea watacheza bila Straika wao Diego Costa ambae yuko Kifungoni baada ya kujilimbikizia Kadi za Njano 5 Msimu huu lakini Eden Hazard, ambae alianzia Benchi kwenye Droo na Watford, huenda akaanza Mechi hii.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumatatu Desemba 28

18:00 Crystal Palace v Swansea
18:00 Everton v Stoke
18:00 Norwich v Aston Villa
18:00 Watford v Tottenham
18:00 West Brom v Newcastle
20:30 Arsenal v Bournemouth
20:30 Man United v Chelsea 

20:30 West Ham v Southampton Jumanne Desemba 29
22:45 Leicester v Man City

Jumatano Desemba 30
22:45 Sunderland v Liverpool

Jumamosi Januari 2
15:45 West Ham v Liverpool
18:00 Arsenal v Newcastle
18:00 Leicester v Bournemouth
18:00 Man United v Swansea
18:00 Norwich v Southampton
18:00 Sunderland v Aston Villa
18:00 West Brom v Stoke
20:30 Watford v Man City

Jumapili Januari 3
16:30 Crystal Palace v Chelsea
19:00 Everton v Tottenham