Saturday, December 12, 2015

FULL TIME: AFC BOURNEMOUTH 2 v 1 MANCHESTER UNITED, JOSHUA KING AITEKETEZA MAN UNITED!

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Joshua King akishangilia bao lake kipindi cha pili dakika ya 54, Bao lililodumu na kuipa Timu yake ushindi.
Joshua King aliipatia bao la ushindi AFC Bournemouth kwa kufanya 2-1 dhidi ya Man United.
Bao la kwanza lilifungwa na Junior Stanislas mapema dakika ya 2.
Mchezaji wa zamani wa Manchester United Joshua King alifunga Bao la ushindi katika Dakika ya 54 wakati Bournemouth ilipoichapa Man United kwenye Mechi ya Ligi Kuu England huko Vitality Stadium.
Bournemouth walingulia kufunga kwa Bao la Dakika ya Pili la Stanislas na Man United kusawazisha Dakika ya 24 kwa Bao la Marouane Fellaini.
Huu ni ushindi wa pili wa kishindo wa Bournemouth baada ya Wiki iliyopita kuifunga Chelsea huko Stamford Bridge.
Kipigo hiki kimehatarisha nafasi ya 4 ya Man United ikiwa Tottenham watashinda Mechi yao ya Leo.
Wakipongezana!