Saturday, December 26, 2015

CHELSEA 2 v 2 WATFORD, OSCAR HAIKOSESHA USHINDI CHELSEA..LEO!


Leo, Chelsea, wakiwa kwao Stamford Bridge, walianza himaya ya Meneja mpya Guus Hiddink kwa Sare.
Chelsea walitangulia kufunga katika Dakika ya 32 kwa Bao la Diego Costa na Watford kusawazisha kwa Penati iliyotolewa baada ya Nemanja Matic kuushika Mpira na Penati hiyo kufungwa na Troy Deeney katika Dakika ya 42.
Watford walikwenda mbele 2-1 kwa Bao la Odion Ighalo la Dakika ya 56 na Diego Costa kufunga Bao lake la Pili Dakika ya 65 na kuipa Chelsea Sare ya 2-2.
Mwishoni Oscar alikosa Penati ambayo ingeweza kuwapa ushindi Chelsea katika Mechi ya kwanza ya Meneja wao mpya Guus Hiddink.