Friday, December 25, 2015

LOUIS VAN GAAL HANA BUDI NI KUIFUNGA STOKE CITY TU LEO! TOFAUTI NA HAPO ITAKUWA NI HABARI NYINGINE.

MENEJA wa Manchester United Louis van Gaal hana njia ya mkato ili kuokoa kibarua chake bali kuifunga Stoke City huko Britannia Stadium hapo Jumamosi, Boksing Dei.
Man United hawajashinda katika Mechi 4 za Ligi Kuu England na Mechi hii na Stoke imechukua umuhimu mkubwa.
Hilo linajulikana na Van Gaal mwenyewe ambae amesema Mechi na Stoke ni lazima washinde.
Van Gaal ameeleza: “Ndio, kama ukipoteza Mechi 3 mfululizo unahitaji ushindi. Tumetilia mkazo kupata ushindi lakini ni kazi ngumu. Stoke City ni wagumu waliifunga hata Man City.”
Mdachi huyo amekiri Stoka ina Wachezaji wazuri hasa Mafowadi wao, Bojan na Xherdan Shaqiri, ambao waliwahi kuzichezea Klabu kubwa za Barcelona na Bayern Munich.
Katika Mechi 15 zilizopita, Man United wamepoteza Mechi 1 tu kwa Stoke.

Hali za Wachezaji
Kwenye Mechi hii, Man United itawakosa Majeruhi Jesse Lingard, Matteo Darmian, Marcos Rojo, Antonio Valencia na Luke Shaw.
Pia, Kiungo Bastian Schweinsteiger hatacheza akiwa anamaliza Kifungo chake cha Mechi 3.
Stoke itawakosa Majeruhi Peter Odemwingie, Marc Muniesa, Stephen Ireland na Shay Given huku Peter Crouch na Geoff Cameron wakiwa na hati hati.