Monday, December 28, 2015

LUCIAN NA FABIAN JOSEPH WATAMBA ARUSHA TOURISM MARATHONAfisa utalii wa tanapa fredy shirima akiwa anamkabidhi zawadi Mwanariadha Reginal Lucian baada ya kushinda kilometa 42,baada ya kukimbia kwa muda wa 1:00:05.

Baadhi ya wanariadha walifanikiwa kupata zawadi katika shindano Arusha tourism Marathon wakiwa katika picha ya pamoja .
Na Woinde Shizza,Arusha
Mwanariadha Reginal Lucian alifanikiwa kushinda kwa upande wa
wanaume,katika shindano la Arusha Tourism Marathon baada ya kutumia muda wa 1:00:05,akifatiliwa na mwanariadha wa kimataifa, Fabian Joseph 1:00:14, nafasi ya tatu,Gabriel Gerald muda wa 1.00.37. katika mashindano hayo ya kilomita 42, yaliyoandaliwa na taasisi la Alfredo Shahanga na Mwanariadha kutoka Kenya, Evance Kiblanget alishika nafasi ya nne baada ya kutumia muda wa 1:07 huku nafasi ya tano ikishinda Wilbart Peter na nafasi ya sita akishindamwanariadha wa kimataifa Dockson Marwa. Kwa upande wa wasichana Angelina Tsere alishinda kwa kutumia musa wa 1:11:17, akifuatiwa na mwanariadha wa kimataifa Mary Naali muda wa 1:11:23, nafasi ya tatu ulikwenda kwa Mkenya Ladis Shemayo aliyetumia muda wa 1:11:37 .
Katika mashindano hayo, ambayo mgeni rasmi alikuwa ni ,Afisa Michezo wa Mkoa wa Arusha,Mwamvita Okeng'o mshindi wa kwanza hadi wa 10 walipewa zawadi.
Viongozi wengine waliotoa zawadi ni pamoja na Katibu Mkuu wa kamati ya Olimpic Tanzania(TOC), Filbert Bayi, Rais wa zamani wa chama cha
riadha nchini(TAAA) Franis John na Afisa Utalii wa TANAPA Fred
Shirika.
Katika mashindano hayo, washindi wa kwanza walipoewa zawadi ta shilingi 500,000, washindi wa pili, 250,000,washindi wa tatu, 200,000, wanne 150,000 na wa tano 100,000 ambapo wa 6 hadi 10 pia walipewa zawadi.


Wakizungumza wakati wa kutoa zawadi, Bayi na Okeng'o walipongeza wanariadha waliojitokeza kwa kuonesha upinzani mkubwa na kutoa wito mashindano haya yafanyike kila mwaka ili kusaidia kukuza utaliiwa ndani. Mkurugenzi wa Alfredo Shahanga kwa upande wake, alisema lengo la mashindano hayo lilikuwa ni kuhamasisha utalii wa ndani, kuhamasisha amani mkoa wa Arusha na kutaka sasa riadha itumike kutangaza utalii.


Mashindano hayo ambayo ni sehemu ya mashindano ya Arusha Tourism
Festival ni mara ya kwanza kufanyika nchini, yalidhamiwa na shirika la
hifadhi za Taifa(TANAPA), kampuni ya vinywaji ya SBC(T) Ltd,radio
Sunrise,BiG Expedetion,Mega Trade Investment,Tanzania Breweris na
Criative Solution.