Saturday, December 12, 2015

MANCHESTER CITY 2 v 1 SWANSEA CITY


MAN CITY Leo wameichapa 2-1 Swansea City ambayo haina Meneja baada ya Garry Monk kutimuliwa na kuongoza Ligi Kuu England.
Man City, wakicheza kwao Etihad, walitangulia kufunga kwa Bao lao Dakika ya 26 kupitia Wilfried Bony na Swansea kusawazisha Dakika ya 90 kwa Bao la Bafetimbi Gomis lakini City wakapata Bao lao la ushindi haraka kufuatia Shuti la Yaya Toure kumbabatiza Kelechi Iheanacho.
Ushindi huu umewafanya City wakae kileleni wakiwa Pointi sawa na Leicester City lakini wao na ubora wa Magoli.
Lakini uongozi huo unaweza kudumu hadi Jumapili wakati Arsenal watakapocheza ugenini na Aston Villa na ushindi kwao utawaweka kileleni pengine hadi Jumatatu Usiku na Leicester kurudi tena kileleni ikiwa wataifunga Chelsea Uwanjani King Power.