Monday, December 28, 2015

MASHABIKI WAPINZANI WAKEBEHI MECHI YA MAN UNITED v CHELSEA, WAIBATIZA JINA LA ‘EL BORINGO’!!

MASHABIKI wa Timu pinzani za Manchester United na Chelsea ambazo Msimu huu zinasuasua kwenye Ligi Kuu England wameikebehi Mechi hiyo ambayo itachezwa Leo Jumatatu Usiku Uwanjani Old Trafford na kuibatiza ‘El Boringo’.
Mechi hii ni ya funga Mwaka ya Ligi Kuu England na inawakutanisha Mabingwa Watetezi Chelsea, ambao Msimu huu wamesambaratika na wako Nafasi ya 15 kwenye Ligi wakiwa Pointi 19 nyuma ya Vinara Leicester City, dhidi ya Man United ambao wako Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 9 nyuma ya Leicester na Pointi 3 nyuma ya Timu ya 4 Tottenham.
Man United, ambao wako Pointi 10 mbele ya Chelsea, wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa hawajashinda katika Mechi zao 7 zilizopita wakiwa pia wamefungwa Mechi 4 mfululizo, 3 zikiwa za Ligi.

Kutokana na hali hiyo, Mashabiki wa Timu pinzani za Man Unite, hasa wale wa Man City, Liverpool na Arsenal, wamevamia Mitandao ya Kijamii, hasa Twitter na kuikebehi Mechi hii na kuibatiza ‘El Boringo” wakimaanisha Mechi Doro, iliyopooza, yaani ‘Boring’ kwa Kiingereza.Van GaalHuko Spain, Mtanange mkali kati ya Mahasimu Real Madrid na Barcelona huitwa ‘El Clasico’ na huko Bundesliga ule wa Bayern Munich na BVB Borussia Dortmund umepachikwa ‘Der Klassiker’ ukitukuza Mechi hizo kubwa lakini hii ‘El Boringo’ ni kebehi kubwa.