Friday, December 25, 2015

MBWANA SAMATTA NJIANI ULAYA JANUARI, KUTUA KRC GENK!

www.bukobasports.comSTRAIKA MAHIRI wa Tanzania anaechezea Klabu ya Congo DR, TP Mazembe Mbwana Samatta yuko njiani kwenda Ulaya kujiunga na Klabu kubwa ya Belgium KRC Genk.
Kwa mujibu wa Jarida la kuaminika la France, L’Equipe, TP Mazembe na Genk wamefikia makubaliano kwa Fowadi huyo hatari kuhamia Genk Mwezi Januari Dirisha la Uhamisho likifunguliwa.
Inaaminika Samatta atasaini Mkataba wa Miaka Minne na Nusu na Genk ambayo inacheza Ligi Kuu ya Belgium iitwayo Belgian Jupiler League na wao wapo Nafasi ya 6 baada ya Kushinda Mechi 8, Sare 4 na Kufungwa 8 Msimu huu.
Msimu huu, Samatta amewika mno Afrika akiwa na TP Mazembe kwa kufunga Bao 8 kwenye CAF CHAMPIONS LIGI na kuwapa Ubingwa wao wa 5 wa Afrika.