Tuesday, December 29, 2015

MCHEZAJI AFUKUZWA BARCELONA MASAA TU BAADA YA KUSAINIWA!

Sergi Guardiola akimwaga winoMASAA machache tu baada ya kusainiwa kuichezea Timu ya Rizevu ya Barcelona huko Spain, Fowadi Sergi Guardiola alifukuzwa kutoka Timu hiyo.
Guardiola, mwenye Miaka 24, alijiunga na Barcelona B Jana Jumatatu na Masaa machache baadae Maofisa wa Barca wakapewa tipu kuwa Mchezaji huyo alitoa posti kwenye Mtandao wa Twitter akiiponda Barcelona na Jimbo la Catalonia ambalo Barca wanaliunga mkono na ambalo linataka kujitenga toka Spain huku pia akiisapoti Real Madrid ambao ni Mahasimu wa Barca.
Guardiola alisajiliwa kutoka Klabu ya Jijini Madrid,, Alcorcon, inayocheza Ligi Daraja la Pili huko Spain, Segunda B.