Saturday, December 26, 2015

FULL TIME: STOKE CITY 2 v 0 MANCHESTER UNITED, BOJAN NA MARKO ARNAUTOVIC WAIPA USHINDI STOKE!

YoungWayne RooneyMeneja wa Stoke CityMan United hii leo imeshushiwa kipigo chake cha 4 mfululuzo na Stoke City walioshinda 2-0 katika Mechi ya Ligi Kuu England na kumfanya kila Shabiki wa Timu hiyo kumchukia Meneja Louis van Gaal na kutaka atimuluwe haraka.
Katika Mechi hii ambayo Kepteni wa Man United Wayne Rooney alianza Benchi, Stoke walifunga Bao lao la kwanza Dakika ya 19 baada ya Pasi ya Geoff Camerok kwa Johnson kunaswa na Mchezaji wa Man United Memphis Depay lakini Kichwa chake hafifu cha kumrudishia Kipa wake De Gea kilitua kwa Johnson ambae haraka alimpasia Bojan Krkic na kufunga Bao laini.
Stoke City walipiga Bao lao la Pili Dakika ya 26 kupitia Marko Arnautovic baada ya Frikiki ya Bojan Krkic kuzuiwa na Ukuta wa Man United na kutua kwake na kuachia Shuti toka Mita 20.
Hadi Mapumziko Stoke 2 Man United Kipindi cha Pili Man United walimtoa Depay na kumuingiza Rooney na kidogo juu na kukosa Bao kadhaa na Mechi kwisha kwa 2-0.
Jumatatu Usiku Man United wako Kwao Old Trafford kucheza na Chelsea katika Mechi nyingine ya Ligi.

Kipindi cha kwanza kimemalizika 2-0 Stoke wanaongoza mpaka sasa.2-0Bojan Krkic dakika ya 19 anaipatia bao la kwanza Stoke City, Bao la pili lilifungwa na Marko Arnautovic dakika ya 26.
VIKOSI:
Manchester United XI (4-2-3-1):
De Gea; Young, Smalling, Jones, Blind; Carrick, Herrera; Mata, Fellaini, Depay; Martial.
Subs: Romero, Varela, McNair, Borthwick-Jackson, Schneiderlin, Pereira, Rooney.

Stoke XI (4-2-3-1): Butland; Johnson, Shawcross, Wollscheid, Pieters; Cameron, Whelan; Shaqiri, Afellay, Arnautovic; Bojan.
Subs: Haugaard, Joselu, Wilson, Van Ginkel, Adam, Diouf, Walters.


Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney amewashauri wachezaji wenzake kukaza buti ili kuokoa kibarua cha meneja wao Louis van Gaal.
Kufuatia kutoshinda katika Mechi 6 zilizopita na kutupwa nje ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kibarua cha Van Gaal kimekuwa kwenye hatari kubwa.
Klabu hiyo imeporomoka hadi nafasi ya 5 kwenye Ligi Kuu England na kujikuta wakiwa na Pointi 9 nyuma ya vinara Leicester City,

Rooney amenukuliwa akisema: "Hatujashinda katika wiki chache zilizopita na ni kawaida kupoteza kujiamini. Inabidi turejeshe imani kwani tuna michezo migumu na tunahitaji tuwe bora zaidi. Si kitu chema kufungwa kila mchezo. Ni ngumu kwa wachezaji. Tunaumia kwani sisi ni watu wa fahari na tunajionea fahari kuichezea Manchester United."Leo tutakazana mkuu!