Monday, December 7, 2015

SANTI CAZORLA NJE MIEZI 3, AFANYIWA OPERESHENI YA GOTI

Meneja  wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha Santi Cazorla atakuwa nje ya Uwanja kwa muda unaoweza kufika Miezi mitatu baada ya kufanyiwa Operesheni ya Goti lake Ijumaa iliyopita.
Cazorla, Mchezaji wa Kimataifa wa Spain mwenye Miaka 30, aliumia Kipindi cha Pili cha Mechi yao ya Ligi Kuu England waliyotoka Sare 1-1 na Norwich City Jumapili Novemba 29 lakini alicheza hadi mwisho.
Wakati huo haikujulikana kama aliumia vibaya lakini baada ya kwenda kwa Mtaalam huko kwao Spain ikagundulika kuna kamba ngumu ya Musuli ndani ya Goti imekatika na alipaswa kufanyiwa upasuaji.
Wenger ameeleza: “Santi alitaka amalize tatizo lake haraka ili apone mapema na akaamua kupasuliwa mara moja. Yule Mtaalam alisema ni wazi lipo tatizo hilo na akashauri upasuaji. Santi akakubali moja kwa moja bila kutafuta ushauri mwingine wa Kidaktari ili asicheldewe kupona haraka!”

Wenger amesema kupona kwa Cazorla kutachukua Miezi 3 au 4 ili arejee Uwanjani na si Msimu wote.
Majeruhi wengine wa muda mrefu wa Arsenal ni Mikel Arteta, Danny Welbeck, Tomas Rosicky na Francis Coquelin.