Wednesday, December 9, 2015

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: VFL WOLFSBURG 3 v 2 MAN UNITED, MAN UNITED HOI! YAONDOLEWA UEFA USIKU HUU..SASA KUSHIRIKI MASHINDANO EUROPA LEAGUE!

Manchester United imefungwa 3-2 na Wolfsburg Bao 3-2 kwenye Mechi ya Kundi B la UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL na kutupwa nje na sasa kucheza Raundi ya Mtoano ya EUROPA LIGI.3-2Kipigo hicho, na ushindi wa PSV Eindhoven wa Bao 2-1 dhidi ya CSKA Moscow, kumezifanya Wolfsburg na PSV kufuzu kwenda Raundi ya Mtoano ya UCL na Man united kumaliza Nafasi ya 3.
Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Wolfsburg kucheza Raundi ya Mtoano ya UCL. 
Naldo akipeta...
Huko Santiago Bernabeu, Cristiano Ronaldo alifunga Bao 4, Karim Benzema kupiga 3 na moja la Mateo Kovacic na kuwapa ushindi Real wa Bao 8-0 toka Kundi A.
Real, na PSG, ambao wameshinda 2-0 walipocheza na Shakhtar Donetsk zote zimesonga na Shakhtar itakwenda EUROPA LIGI.

Man City, ambao walikuwa washafuzu toka Kundi D, Leo wameichapa Borussia Mönchengladbach 4-2 na kumaliza kileleni mwa Kundi hilo na kufuatiwa na Juventus ambao Leo walifungwa 1-0 na Sevilla ambao wamemaliza Nafasi ya 3 na hivyo kwenda EUROPA LIGI.
Van Gaal akipagawa baada ya kutupwa njeNaldo ndiye aliyepeleka kilio baada ya kufunga bao la tatu kwa WolfsburgNaldo akitupia kwa kichwa mpira wa konaAkitupia bao la piliMata akishangilia baoMan United wakipongezana...Akishangilia bao1-1Raha ya kufunga bao!Kikosi cha Man United Van Gaal Mwenyekiti!Sir Alex Ferguson Sir BobbyMapema kabla ya Mechi walipokuwa wanapasha