Tuesday, December 15, 2015

UEFA YATANGAZA MAREFA 18 KWA FAINALI ZA EURO 2016!

KAMATI ya Marefa ya UEFA imeteua Marefa 18 ambao watasimamia Mechi 51 za Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, zitakazochezwa Nchi France Makani.
Kama ilivyokuwa kwa EURO 2012 na Mechi za kufuzu Fainali za UEFA EURO 2016, Mechi 1 itachezwa na Refa akisaidiwa na Wasaidizi Wawili wa pembeni mwa Uwanja na Wawili kwenye Mstari wa nyuma ya Magoli.
Wengi wa Marefa Wasaidizi watatoka Nchi moja na Refa wa Mechi.
Listi ya mwisho ya Marefa kwa ajili ya Fainali za EURO 2016 itathibitishwa Februari 2016.
LISTI KAMILI:
Martin Atkinson (England)
Felix Brych (Germany)
Cüneyt Çakir (Turkey)
Mark Clattenburg (England)
William Collum (Scotland)
Jonas Eriksson (Sweden)
Ovidiu Hategan (Romania)
Sergey Karasev (Russia)
Viktor Kassai (Hungary)
Pavel Královec (Czech Republic)
Björn Kuipers (Netherlands)
Szymon Marciniak (Poland)
Milorad Mažić (Serbia)
Svein Moen (Norway)
Nicola Rizzoli (Italy)
Damir Skomina (Slovenia)
Clément Turpin (France)
Carlos Velasco Carballo (Spain)