Sunday, December 27, 2015

VIPIGO VYAMTISHA VAN GAAL, ANENA SASA....ASEMA SASA ANAWEZA KUAMUA KUNG'OKA MWENYEWE OLD TRAFFORD"

MENEJA  wa Manchester United Louis van Gaal amesema anaweza kuamua kwa hiari yake kuachia ngazi baada ya Jana kupokea kipigo cha 4 mfululizo huko Britannia Stadium walipochapwa 2-0 na Stoke City.
Huku kukiwa na uvumi mkubwa kwa Mdachi huyo ambae Kikosi chake hakijashinda katika Mechi 7 kuwa atafukuzwa, Jana akihojiwa na Wanahabari baada ya Mechi hiyo ambayo walishushwa hadi Nafasi ya 6 kwenye Ligi Kuu England, aliulizwa ikiwa anahofia kufukuzwa.

Van Gaal alijibu: "Hilo ni jambo nitajadiliana na Ed Woodward (Mtendaji Mkuu wa Man United) na si wewe!"
Van Gaal aliongeza: "Si lazima Siku zote Klabu ikufukuze. Wakati mwingine unaweza kuamua mwenyewe. Lakini mimi nataka kwanza kuongea na Bodi ya Man United, Wafanyakazi na Wachezaji lakini si nyinyi!"
Mechi inayofuata kwa Man United ni Uwanjani Old Trafford Jumatatu Usiku dhidi ya Mabingwa Watetezi Chelsea ambao nao Msimu huu wako taabani kiasi cha Wiki iliyopita kumfukuza Meneja wao Jose Mourinho na kumteua Guus Hiddink kama Meneja wa muda hadi mwishoni mwa Msimu.