Sunday, December 6, 2015

YAMOTO BENDI WAINGIA TUZO ZA KORA

Waimbaji wa yamoto bendi wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Mwandishi Mwetu
WAKATI jana wakiendelea kutoa burudani katika mji wa Washington DC, Bendi ya Yamoto, imeingia katika kuwania tuzo za Kora 2016, ikiingia katika kipengele cha Most Promising Male Artist Of Africa. Mkurugenzi wa bendi hiyo Said Fella, alisema kwanza anamshukuru Mungu vijana wake juzi usiku walikuwa na onesho lao la pili lililofanyika Washington DC na kuweza kufanya vizuri, lakini la pili kuingia katik tuzo za Kora. Fella ambaye ni diwani wa Kata ya Kilungule alisema ni kitu kikubwa sana kwake