Thursday, January 7, 2016

ADNAN JANUŹAJ ARUDI MANCHESTER UNITED TOKA DORTMUND!

Man United imeamua kumrudisha Mchezaji wao Adnan Januzaj kutoka Borussia Dortmund ambako alikuwa kwa Mkopo wa Msimu mmoja.
Man United wameiamuru Dortmund kumrejesha Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Belgium mwenye Miaka 20 kutokana na kutopewa Mechi za kucheza kitu ambacho ni tofauti na lengo la Mkopo huo la kumkomaza na kumpa uzoefu kwa kucheza Mechi nyingi.
Akiwa na Dortmund tangu mwanzoni mwa Msimu huu, Januzaj alicheza Mechi 12 tu na kuanza 3 tu kati ya hizo.
Kwenye Bundesliga, Januzaj amecheza Mechi 6 tu na zote alitokea Benchi na tangu Desemba 10, alipocheza Mechi ya Europa Ligi ambayo Dortmund walifungwa na PAOK Salonika, Januzaj hajacheza tena.
Mwanzoni mwa Msimu huu, Januzaj ambae Mkataba wake unakwisha 2018, aliichezea Man United Mechi 4 Mwezi Agosti na kufunga Bao la ushindi dhidi ya Aston Villa.