Tuesday, January 5, 2016

CAPITAL ONE CUP: STOKE CITY 0 v 1 LIVERPOOL, IBE AIPA USHINDI LIVERPOOL

Ibe dakika ya 37 kaipachikia bao Liverpool baada ya kuunganisha mpira uliopigwa kama kona na Firmino kuugusa kwa kuunganisha pasi kwa aliyemaliza kwa shuti kali langoni Ibe.
Liverpool wamepata ushindi wa Ugenini wa Bao 1-0 walipoifunga Stoke City Bao 1-0 huko Britannia Stadium katika Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya C1C, Capital One Cup, ambalo ni Kombe la Ligi.
Bao la ushindi la Liverpool lilifungwa na Jordon Ibe katika Dakika ya 37.
Ibe aliingizwa kumbadili Philippe Coutinho alieumia Musuli za Pajani.
Stoke, ambao hivi karibuni walizifunga Chelsea, Manchester City na Manchester United Uwanjani kwao hapo Britannia, walishindwa kurudia fomu yao hiyo walipocheza na Liverpool na sasa wana Mlima mrefu kushinda huko Anfield katika marudiano.
Timu hizi zitarudiana huko Anfield hapo Januari 26.
Nusu Fainali nyingine itachezwa Leo Jumatano Usiku huko Goodison Park kati ya Everton na Man City na marudiano yake ni huko Etihad hapo Januari 27.

Benteke nje! Roberto Firmino kaanzaVIKOSI:
Stoke XI:
Butland, Johnson, Shawcross, Wollsheid, Pieters, Cameron, Whelan, Affelay, Shaqiri, Arnautovic, Bojan.

Subs: Haugaard, Joselu, Wilson, Van Ginkel, Adam, Walters, Crouch.

Liverpool XI: Mignolet, Clyne, Toure, Lovren, Moreno, Lucas, Can, Allen, Coutinho, Lallana, Firmino.
Subs: Bogdan, Milner, Benteke, Brannagan, Ibe, Smith, Randall.

Mechi za kwanza za nusu fainali ya Capital One Cup, ambalo ni Kombe la Ligi huko England, zitachezwa leo Jumanne Usiku Januari 5 na Jumatano Januari 6.
Leo Jumanne Stoke City watakuwa nyumbani Britannia kuwakaribisha Liverpool na kesho Jumatano Everton watakuwa Goodison Park na Man City.
Nusu Fainali za michuano hiyo zitachezwa kwa mikondo miwili ya nyumbani na ugenini na timu zitarudiana tena hapo Januari 26 na 27.
Timu ambazo zimetinga hatua ya nusu fainali ni Stoke baada ya kuibwaga Sheffield Wednesday na Liverpool kuitoa Southampton wakati Everton waliwatoa Middlesbrough na Man City wakiitupa nje Hull City.
Bingwa Mtetezi wa Kombe hili alikuwa Chelsea ambae alitupwa nje na Stoke City kwa Mikwaju ya Penati 5-4 baada ya Sare ya 1-1.