Saturday, January 16, 2016

CHELSEA, WEST BROM ZAFUNGULIWA MASHITAKA NA FA

Chelsea na West Bromwich Albion zimefunguliwa Mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kutokana na utovu wa nidhamu wa Wachezaji wao kwenye Mechi ya Jumatano iliyopita waliyotoka Sare 2-2.
Mashitaka hayo yanatokana na jinsi Wachezaji walivyokwaruzana mara baada ya Kiungo wa WBA, Claudio Yacob, kumchezea Rafu Diego Costa na Refa kutompa Kadi ya Njano ya pili.
FA imedai Klabu hizo mbili zimeshindwa kudhibiti Wachezaji wao na kufanya utovu wa nidhamu.
Klabu hizo zimepewa hadi Jumatano Januari 20 Saa 3 Usiku, kwa Saa za Bongo, kukiri au kukana Mashitaka yao.
Akiongea hapo Jana, Meneja wa muda wa Chelsea, Guus Hiddink, alisema anaamini Yacob alipaswa kupewa Kadi ya Njano ya pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

Hiddink alieleza: “Wakati wa tukio lile nilimwendea Refa wa Akiba Jon Moss na kumwambia huyu Refa ni mbovu kupita wote katika Ligi Kuu nay eye akanijibu-bado hujaniona mimi! Nadhani lilikuwa jibu zuri mno!”