Tuesday, January 19, 2016

CHRIS SMALLING AMWAGIA SIFA KEPTENI WAO WAYNE ROONEY

CHRIS SMALLING amemsifia Kepteni wao wa Manchester United Wayne Rooney kwa kurejea tena na kuanza kufunga Magoli na pia kuwaponda waliomkandya na kumfuta kwa kudai amekwisha.
Juzi huko Anfield, Rooney alifunga Bao la ushindi Dakika ya 78 wakati Man United wanaichapa Liverpool 1-0 na hilo lilikuwa Bao la Kihistoria.
Mbali ya kuwa lilikuwa Bao la kwanza la Rooney Uwanjani Anfield tangu 2005, pia lilikuwa Bao la 100 kwa Man United kuifunga Liverpool Uwanjani Anfield na vile vile lilikuwa Bao la 176 kwa Rooney kufunga katika Ligi Kuu England na kumfanya awe ndio Mfungaji Bao nyingi katika Ligi hiyo akiwa na Klabu moja tu.
Awali Rekodi hiyo ilishikiliwa na Thierry Henry aliefunga Bao 175 akiwa na Arsenal pekee.

Hivi sasa Rooney ameipigia Man United Bao 5 katika Mechi 4 zilizokwisha na kufuta ule mwendo mbovu wa kabla ya hapo alipofunga Bao 1 tu katika Mechi 13 za Mashindano yote.
Smalling anaamini Rooney alinufaika kwa kupigwa Benchi kwenye Mechi na Stoke City Siku ya Boksing, Desemba 26.
Smalling ameeleza: "Tangu Gemu hiyo Rooney amerejea na kuonyesha yeye ni Mchezaji wa juu. Kuachwa kulimpa motisha na Mastraika hupitia vipindi vya ukame lakini wale bora hurudia kufunga na kuendelea kufunga mfululizo!"
"Wazza yuko hivi. Msimfute!"