Wednesday, January 13, 2016

CITY WAPATA PIGO NAHODHA WAO VINCENT KOMPANY NJE WA MUDA MREFU!

MBIO za Manchester City kutwaa Ubingwa Msimu huu zinaelekea kupata pigo kubwa baada ya kutobolewa kuwa Kepteni wao Vincent Kompany atakuwa nje ya Uwanja kwa muda mrefu kupita ilivyokadiriwa akisumbuliwa na Misuli ya Mguuni.
Kompany, mwenye Miaka 29, Msimu huu ameichezea City Mechi 12 tu kutokana na kuandamwa mfululizo na tatizo hilo hilo la Musuli za Mguuni.
Mara ya mwisho kuumia kwa Beki huyo ambae pia huchezea Timu ya Taifa ya Belgium ni Desemba 26 walipoifunga Sunderland 4-1 na awali ilitegemewa atakuwa nje kwa Wiki 4 tu lakini Meneja wa City, Manuel Pellegrini, amebainisha sasa wanategemea atakuwa nje kwa muda mrefu zaidi.

MBIO za Manchester City kutwaa Ubingwa Msimu huu zinaelekea kupata pigo kubwa baada ya kutobolewa kuwa Kepteni wao Vincent Kompany atakuwa nje ya Uwanja kwa muda mrefu kupita ilivyokadiriwa akisumbuliwa na Misuli ya Mguuni. Pellegrini alifafanua kuwa hadi sasa wanachunguza zaidi kwanini Kompany anapata maumivu hayo hayo mara kwa mara ambayo wanadhani yatamweka nje hadi Msimu ukielekea ukingoni.
Kukosekana kwa Kompany ni wazi ni pigo kubwa kwa City katika mbio zao za kusaka Ubingwa kwani takwimu zinadhihirisha kuwa City ilifungwa Bao 1 tu kwenye Ligi wakati yeye akiwepo Uwanjani lakini wamekuwa wakitobolewa kila Mechi katika Mechi 11 ambazo alikosa kucheza kasoro 1 tu kati ya hizo ambayo ndiyo hawakufungwa hata Bao.
Mbali ya kumkosa Kompany, City pia itamkosa Sentahafu wao mwingine, Eliaquim Mangala, kutokana na tatizo la Musuli za Pajani lakini Pellegrini amesema hataingia Sokoni hii Januari wakati Dirisha la Uhamisho liko wazi ili kuziba mapengo hayo.
Pellegrini ameeleza: “Tunae Martin Demichellis, tunae Nicolas Otamendi, yupo Bacary Sagna ambae huweza kucheza Sentahafu na yupo Chipukizi Cameron Humphreys. Mangala atarejea hivi karibuni hivyo hatufikirii mabadiliko.”
City, ambao Jumatano Usiku wako kwao Etihad kucheza na Everton kwenye Ligi, wapo Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 3 nyuma ya Vinara Arsenal na 1 nyuma ya Timu ya Pili Leicester City.