Sunday, January 31, 2016

DROO RAUNDI YA 5 EMIRATES FA CUP YAFANYIKA, CHELSEA vs MAN CITY, SHREWSBURY vs MAN UNITED, ARSENAL vs HULL CITY

DROO ya Mechi za Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP imefanyika na kuzua Bigi Mechi kati ya Chelsea na Man City wakati Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, Arsenal, wakiwa Nyumbani kucheza na Hull City.
Man United wako Ugenini kucheza na Timu ya Daraja la chini Shrewsbury Town.
Zipo Mechi za Timu za Ligi Kuu England pekee ambapo Tottenham wako kwao kucheza na Crystal Palace na Bournemouth kuivaa Everton.

DROO YA RAUNDI YA 5
Mechi kuchezwa Wikiendi ya Februari 20 hadi 22

Chelsea v Manchester City
Reading v West Brom au Peterborough
Watford v Leeds United
Shrewsbury Town v Manchester United
Blackburn v Liverpool au West Ham
Tottenham v Crystal Palace
Arsenal v Hull
Bournemouth v Everton

THE EMIRATES FA CUP 2015/16
TAREHE MUHIMU
Raundi ya 3
Ijumaa 9 Januari 2016

Raundi ya 4
Jumamosi 30 Januari 2016
Raundi ya 5
Jumamosi 20 Februari 2016
Raundi ya 6-Robo Fainali
Jumamosi 12 Machi 2016

Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali Jumamosi 21 Mei 2016